Mwimbaji Akoth Esther, anayejulikana kama Akothee, amefunguka kuhusu sababu ya kuongezeka kwake uzani.
Akothee alisema kuwa uvimbe wake ni matokeo ya ugonjwa ambao anapambana nao kwa sasa. Alizidi kufichua kuwa aliogopa kwenda kulala kwa sababu anaamka akiwa hajisikii vizuri mara nyingi.
Pia aliwaonya watu kutozungumzia uzito wake anapokutana nao.
“Usikutane na mimi na kuanza kuniambia jinsi nilivyo mnene. Nina hali ya afya. Nimevimba kwa sababu ya kuhangaika na maumivu ya kukosa usingizi. Naogopa kwenda kulala maana ninaamka na ganzi kwenye vidole vyangu, hali hii inanitisha” alisema Akothee.
Chapisho lake linakuja wiki kadhaa baada ya kufichua kwamba alilazwa hospitalini kwa sababu ya mshipa wa neva. Mpenzi wake Nelly Oaks alikuwa hospitalini naye muda mwingi, na aliendelea kuwapa mashabiki sasisho kuhusu hali yake.
Comments
Post a Comment