Mwigizaji wa Tanzania, Jacqueline Wolper hivi karibuni aliwajibu mashabiki wanaoendelea kumtaka asimfanye mwanae kuvaa cheni za dhahabu.
Wolper ameshare screenshot ya ujumbe kutoka kwa shabiki, na ndani yake shabiki huyo alimwambia kuwa ni dhambi kwa mtoto wa kiume kuvaa dhahabu. Alimjibu shabiki huyo na kusema kuwa yeye na mumewe ni Wakristo na hawazingatii sheria za Kiislamu.
The fan wrote, “ Sikufundishi ila nakukumbusha dhahabu inaregeza mwili kwa mtoto wa kiume sio nzuri ndio mana sisi waislam nisunna silva kwa mwanaume n mtoto akianza kuota meno tunamvisha silver iwe kidani au pete. Asante nimekuambia ila sio kwa ubaya mama"
Kwa hili Wolper akajibu, “Mimi sio muislam ni mkristo na babaake pia nimkresto mwaya”
Wolper aliongeza kuwa ujumbe huo ulikuwa kwa wale wote ambao wamekuwa wakimwambia kitu kimoja. Kwa hivyo, hawapaswi kumsumbua tena.
“Jibu la wote hilo natumaini. Amtonishauri tena sawa” Aliongeza.
Comments
Post a Comment