Mange alimpongeza Tanasha kwa kupata na mwimbaji huyo wa Nigeria kupitia Instagram yake. Pia aliwaambia mashabiki wake kwamba Tanasha na Omah Lay wanadaiwa wako Mombasa, wakifurahia wakati mzuri pamoja.
Mange aliongeza kuwa hivi karibuni Tanasha atavaa nguo za wabunifu kwa sababu wanamuziki wa Nigeria wana pesa nyingi.
“Usicheze na msichana wangu Tanasha. Amejipanga kwa muda mrefu. Ako zake na mnaigeria sasa. Ako na Omah Lay. @omah_lay . Si mnajua pesa za wanamuziki wa Nigeria ni ndefuuu, sasa hivi Tanasha ataanza vaa Magucci na ma Chanel” aliandika Mange pamoja na kolagi ya picha ya Tanasha na mwimbaji huyo wa Nigeria.
“Dakika hii naandika hii posti wako Mombasa wanakula raha. Hivi mnajua ma ex wa Dai wote wame level up, alishindwa kulevel up ni Bi Tukinao tu” she added.
Omah Lay ndiye mwanaume wa kwanza kuhusishwa kimapenzi na Tanasha Donna tangu alipoachana na Mwimbaji wa Tanzania Diamond Platnumz, baba wa mtoto wake Naseeb Junior.
Comments
Post a Comment