Mwimbaji wa Nigeria, Damini Ebunoluwa, anayejulikana kitaaluma kama Burna Boy, amezungumzia tena uvumi kuhusu kuhusika kwake katika ufyatulianaji wa risasi uliotokea kwenye klabu ya Cubana mwaka uliopita. Katika wimbo wake mpya uitwao "Thanks" akiwa na Rapa wa Marekani J Cole, Burnaboy anarejelea tukio hilo na kuhoji kwa nini baadhi ya Wanigeria wanataka kumwona akishindwa ilhali anashinda tuzo kwa nchi yake na kuinua hadhi yake kwenye jukwaa la kimataifa. Katika wimbo huo Burna Boy anasema , “You say that I'm cancelled again. You say I shoot pesin for Cubana/ Because I wan collect pesin woman (That's how they act, right?). Is this the m*****king thanks I get for making my people proud every chance I get?” Unasema nimekataliwa tena. Unasema nilimpiga mtu risasi kwenye Cubana/ Kwa sababu nataka mwanamke wa mtu (Ndivyo wanavyotenda, sivyo?). Je, hii ndiyo shukrani ninazopata kwa kufanya watu wangu wajivunie kila nafasi ninayopata?” Mnamo 2022, Burna Boy alika...
Home of East Africa Entertainment, Politics and Celebrity news